Taarifa na Sammy Kamande.
Kasisi wa Kanisa la Kianglikana la St. Pauls Kiembeni eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa, Tom Dawa amewahimiza viongozi wa kidini kuendeleza tamaduni katika Makanisa yao.
Akizungumza wakati wa sherehe ya kitamaduni zilizoyaleta pamoja makabila 7 kote nchini, Dawa ametaja hatua hiyo kama itakayomaliza migawanyiko miongoni mwa waumini wa makanisa mbali mbali nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Bodi ya halmashauri ya maendeleo Pwani Beatrice Gambo, amesema mfumo huo ni mwafaka katika kujenga ushirikiano baina ya jamii na makanisa.
Miongoni mwa jamii zilizowakilishwa katika halfa hiyo ni wamijikenda, wataita, wakamba, wakikuyu, wabaluhya na waluo.