Story by our Correspondents –
Jaji mkuu nchini Bi Martha Koome amewapisha rasmi makamishna wanne wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC baada ya kuidhinishwa rasmi bunge la kitaifa.
Katika halfa hiyo iliyoongozwa na Msajili mkuu wa Mahakama nchini Bi Anne Amadi na kuandaliwa katika majengo ya Mahakama ya upeo, Jaji Koome amewashauri makamishna hao kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba.
Jaji Koome amewataka makamishna hao waliokula kiapo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa haki na uwazi, akisema hatua hiyo ndio itakayofanikisha uchaguzi huru na haki.
Makamishna hao waliokula kiapo ni pamoja na Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit, na Justus Abonyo.