Story by Our Corresponents-
Makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC wamefika mbele ya Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu haki na sheria JLAC kujitetea dhidi ya hoja ya kushinikiza kutimuliwa kwao afisini.
Makamishna hao akiwemo Naibu Mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherera, Kamishna Irene Masit, Francis Wanderi na Justus Nyangaya wanadaiwa kuenda kinyume na katiba kwa kupinga matokeo ya urais ya uchaguzi wa Agosti 9 licha ya kufahamu wazi kwamba uchaguzi ulizingatia kanuni zote.
Mawakili wa makamishna hao, wakiongozwa na Wakili Jotham Arwa na Danstan Omari wamewatetea wateja wao wakidai kwamba hoja iliyowasilisha bungeni kutaka kuwatimua afisini makamishna hao haina uzito wowote bali imechochewa kisiasa.
Hata hivyo kikao hicho limelazimika kisitishwa pale viongozi wa upinzani katika kamati hiyo wakiongozwa na Kiranja wa wachache bungeni ambaye pia na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed kupendekeza kikao hicho kuwa cha faraga kutoka na uzito wa swala hilo.
Kiongozi wa upanzani nchini Raila Odinga, Martha Karua, Kalonzo Musyoka, Wakili Makau Mutua, ni kati ya viongozi waliofika bungeni kuzikilia kikao hicho cha kuwahoji makamishna hao.