Picha kwa hisani –
Makachero wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC wamevamia nyumba na afisi za gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru zilizopo kaunti za Kirinyaga na Nairobi.
Maafisa hao wamevamia maeneo hayo mwendo wa saa kumi na mbili asubui ya leo ili kusaka stakabadhi muhimu zinazohusu madai ya ufisadi yanayomkabili Waiguru,upekuzi ambao umedumu kwa masaa kadhaa.
Makachero wa EACC waliotekeleza upekuzi huo wameweka wazi kwamba wamekabidhiwa kibali na mahakama kufanya hivyo ili kufanikisha uchunguzi wao kuhusu kesi hizo.
Hatua hio imejiri mwezi mmoja tu baada ya bunge la seneti kumuondolea Gavana Waiguru madai ya ufisa na utumizi mbaya wa afisi shutuma zilizoibuliwa na wawakilishi wadi wa Kirinyaga