Picha kwa hisani –
Zoezi la kunyunyiza dawa majengo ya mahakama ya mjini Kwale linaendelea baada ya wafanyikazi watano wa Mahakama hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya corona.
Waziri wa afya katika kaunti ya Kwale Francis Gwama wagonjwa hao wa tano wa corona kwa sasa wanaendelea na matibabu wakiwa nyumbani akiwataka wakaazi kuzidi kuchukua tahadhari ili kukwepa maambukizi.
Hata hivyo mahakama hio ya Kwale imewasihi wakaazi wa kaunti hio kuwasilisha kesi zao katika mahakama za Msambweni na Mombasa hadi pale mahakama yak wale itakaporejelea vikao vyake.
Mahakama hio ya Kwale itasalia kufungwa kwa siku kumi na kurejelea vikao vyake tarehe 23 ya mwezi huu wa Novemba.