Picha kwa Hisani –
Jaji mkuu nchini David Maraga ameteua majaji watano watakaosikiliza kesi zilizowasilishwa mahakamani zinazohusiana na kuvunjwa kwa bunge.
Majaji hao ni pamoja na jaji Lydia Achode,Jaji George Odunga,James Makau,Jaji Anthony Ndungu na Pauline Nyamweya.
Kufikia sasa kuna kesi sita zilizowasilishwa mahakamni za kutaka kuvunjwa kwa bunge kwa misingi kwamba limeshindwa kupitisha sheria ya tuluthi mbili ya usawa wa jinsia.
Mbali na kesi hizo tayari kuna kesi iliowasilishwa na wakenya wawili ya kupinga ushauri wa maraga kwa rais Uhuru Kenyatta wa kutaka kuvunjwa kwa bunge na kesi sawa na hio iliwasilishwa na mwanasheria mkuu nchini Paul Kihara.