Picha kwa hisani –
Jaji anayeongoza uchunguzi wa ufisadi nchini Afrika Kusini amesema kuwa malalamiko ya ufisadi yatawasilishwa dhidi ya Rais Jacob Zuma baada ya kuondoka nje ya kikao cha kamati kilichokuwa kikifanya uchunguzi dhidi yake.
Zuma alijaribu kuhakikisha Naibu Jaji Raymond Zoro anaondolewa katika uchunguzi huo, akimtuhumu kuwa na upendeleo.
Lakini wakati lengo lake lilipogonga mwamba, rais huyo wa zamani na wakili wake hawakurejea tena mbele ya kikao hicho kukabiliana na maswali kuhusu ufisadi.
Kamati, ambayo imekuwa ikisikiliza ushahidi tangu mwaka 2018, imesema kuwa iliwasiliana mara moja na Mahakama ya juu zaidi ya Afrika Kusini, Mahakama ya Katiba, katika juhudi za kumlazimisha Zuma aitikie wito wa kuhojiwa.