Story by Ali Chete-
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu katika kaunti ya Mombasa wameitaka idara ya mahakama kuweka mikakati ya kutosha ili kuhakikisha kesi za dhulma za kijinsia zinapewa kipaumbele mahakamani.
Wakiongozwa na Afisa wa maswala ya dharura katika Shirika la Haki Afria Alexander Mbela, wanaharakati hao wameitaka idara hiyo kuhakikisha waathiriwa wa dhulma hizo wanapata haki.
Mbela amesema tayari shirika hilo linaendeleza kampeni za kuwahamasisha wanawake kufahamu haki zao hasa ili kupinga dhulma hizo.