Mwanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT aliyepigwa risasi na kujeruhiwa baada ya kuruka juu ya ua la Ikulu ameachiliwa huru kwa dhama ya KSh 100,000.
Hata hivyo, alipofikishwa mbele ya Hakimu Francis Andayi Alhamisi Julai 4, Brian Bera hakujibu mashtaka dhidi yake.
Hakimu huyo alimuachilia kwa masharti kuwa babake atampeleka kwa matibabu ya kiakili katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi. Mahakama ilitenga Agosti 7, kama tarehe ya kujibu mashtaka baada ya hospitali ya ripoti ya matibabu kutolewa.
Wakati Bera alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Jumatano Julai 3, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika kitivo cha handisi alimwomba radhi Rais Uhuru Kenyatta kwa kosa alilofanya.