Taarifa na Mimuh Mohamed
Nairobi, Kenya, Julai 18 – Mahakama kuu imeagiza kesi iliowasilishwa mahakamani na Maseneta dhidi ya bunge la kitaifa ya kupinga kupitisha sheria 24 kwa njia inayokiuka katiba ya nchini, kusikizwa kama ya dharura
Akitoa uamuzi huo jaji wa mahakama kuu Weldon Korir amesema kesi hiyo imeibua masuala yenye uzito na inafaa kupewa kipau mbele.
Jaji Korir ameagiza kesi hio kuwasilishwa mbele ya jaji mkuu nchini David Maraga ili aunde jopo la majaji watatu wa kusikiliza kesi hiyo.
Katika kesi hiyo iliowasilishwa mahakamani na Spika wa bunge la seneti Kenneth Lusaka, kiongozi wa walio wengi bunge la seneti Kipchumba Murkomen pamoja James Orengo, maseneta wamedai kwamba wabunge walipitisha sheria hizo pasi na kuwahusisha hali iliyo kinyume na katiba ya nchi.