Wakazi wa wadi ya Ganda eneo bunge la Malindi sasa watalazimika kurudi tena debeni kumchagua mwakilishi wa wadi hiyo baada ya spika wa bunge la kaunti ya kilifi Jimmy Kahindi kutangaza wazi nyadhfa hiyo.
Akiongea na wanahabari mjini Malindi Kahindi amesema kuwa amepata amri kutoka kwa mahakama kuu ya Malindi inayoweka wazi kwamba uchaguzi huo unafaa kurudiwa kwani haukufanywa kwa uwazi.
Kahindi aidha amesema kuwa mwakilishi wa sasa wa wadi hio Abdulrehman Omar sio mwakilishi tena wa bunge la kaunti ya Kilifi na kumtaka kujitenga na huduma za bunge hilo.
Kahindi sasa ameweka wazi kuwa tume ya uchanguzi nchini IEBC italazimika kuandaa uchaguzi mpya ndani ya siku tisini zijazo.
Ushindi wa mwakilishi huyo wa wadi ya Ganda ulibatilishwa mwezi jana na mahakama kuu ya Malindi na kuamuru tume ya uchaguzi kuandaa uchaguzi mdogo wa nyadhfa hio.
Omar ambaye alitetea kiti hicho kupitia chama cha ODM atalazimika kumenyana na wapinzani wake wa karibu akiwemo Joseph Kiponda wa chama cha Jubilee na Reuben Katana wa chama cha Kadu Asili.
Taarifa na Charo Banda.