Taarifa na Charo Banda.
Malindi, Kenya, Julai 18 – Idara ya mahakama nchini imeanzisha mpango wa kusikiza kesi zilizowasilishwa mahakamani kupitia njia ya upatanisho ili kupunguza mrundiko wa kesi katika mahakam za humu nchini.
Kulingana na msajili wa mahakama nchini, Judith Omange kwa sasa kuna zaidi ya kesi elfu 90 katika mahakama za humu nchini zinazosubiri kusikizwa.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mpango huo mjini malindi Jaji wa mahakama ya mazingira na ardhi James Olola amesema kuwa mpango huo utaleta afueni hata kwa majaji na mahakimu wanaoshughulikia kesi mbali mbali.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi, ameupongeza mpango huo akisema kuwa wananchi sasa watapata fursa ya kujieleza na kupata haki.
Tayari mpango huo umeanzishwa katika kaunti mbali mbali nchini ikiwemo kaunti za Lamu, Nyeri, Nairobi na Kisumu ambapo tayari asilimia 60 ya kesi zimetatuliwa kupitia mpango huo wa upatanishi.