Story by Our Correspondents-
Jopo la Majaji 7 wa Mahakama ya upeo wakiongozwa na Jaji mkuu nchini Martha Koome wameharamisha mchakato wa BBI wakisema ni kinyume cha Katiba.
Akisomo uamuzi wa pamoja wa majaji hao, Jaji Koome ameelezea kwa kifupi uamuzi wa majaji wenzake akisema BBI ilikosa kuzingatia vikao vya umma, Rais hana mamlaka ya kuchangia mchakato wa BBI, IEBC ilikosa idadi hitajika ya Makamishna wa kukagua saini za BBI na mfumo ulitumika wa kubuni BBI ulikiuka vipengele vya Katiba.
Katika uamuzi wake Jaji Isaac Lenaola, amesema rais hawezi kuidhinisha mchakato wa marekebisho ya Katiba kwani jukumu hilo liko chini ya wananchi, pendekezo la kubuniwa kwa maeneo bunge 70 ni kinyume cha katiba na IEBC haikuwa na idadi kamili ya kuamua kufanyika kwa referendum.
Kwa upande wake Jaji Njoki Ndungu, amesema Rais alikosea pakubwa kwa kuteua kamati ya BBI, na BBI haikuwa na swali maalum la Refurendem huku akipinga uamuzi wa Mahakama kuu kwamba rais alikuwa mshawishi mkuu katika BBI na kusema ushawishi wa BBI unaitaji idadi ya wananchi.
Naye Jaji William Ouko katika uamuzi wake, amepinga uamuzi wa mahakama ya kuu na ile ya Rufaa kwamba hakuwa na ushahidi wa kutosha wa viongozi wa BBI kufanya vikao vya umma, huku akiunga mkono kwamba IEBC ilikuwa na idadi sawa kikatiba ya kukagua saini za BBI.
Hata hivyo Jaji Smokin Wanjala katika uamuzi wake amesema rais hawezi kushtakiwa akiwa ofisini, viongozi wa BBI walikosa kuweka vikao vya umma huku akisema muundo msingi ulitumika uliotumika kubuni BBI ulikosa kuzingatiwa vipengele vya katiba.
Hata hivyo baadhi ya wakenya waliokuwa wakifuatilia vikao hivyo vya mahakama wameunga mkono uamuzi wa Mahakama kutupilia mbali mchakato wa BBI huku wakisema wakikosoa uamuazi huo Mahakama.