Story by: Taalia Kwekwe
Mahakama ya Mombasa imeipa muda zaidi idara ya polisi nchini kukamilisha uchunguzi dhidi ya kesi ya mauaji inayomuandama mwanamume mmoja wa umri wa miaka 20.
Mahakama imeelezwa kwamba shtakiwa kwa jina Abdulaziz Swaleh, alitekeleza mauaji hayo baada ya kumtaka shingo nyanya yake mwenye umri wa 80 mnano tarehe 21 mwezi Januari mwaka huu katika eneo la mji wa Kale kaunti ya Mombasa.
Hakimu mkuu wa Mahakama hiyo Vincent Adet ameagiza mshtakiwa kufanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kurejeshwa tena Mahakamani
Hata hivyo kesi hiyo itatajwa mnamo tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu.