Story by Our Correspondents-
Mahakama kuu mjini Mombasa imefutilia mbali kesi ya mauaji iliyokuwa ikimuandama Waziri wa Jinsia na utumishi wa umma Aisha Jumwa.
Hatua hiyo imejiri baada ya Ofisi ya mkurugenzi wa Mashtaka ya umma nchini ODPP kuandikia barau Mahakama kuu ya Mombasa ikiomba kuiondoa kesi hiyo ya mauaji dhidi ya Jumwa.
Jaji wa Mahakama hiyo Ann Onginjo amesema kuondolewa kwa kesi hiyo ya mauaji dhidi ya Jumwa kwa kuzingatia kifungu cha 87 ibara ya kwanza {a} sio kizuizi cha Mahakama kufungulia upya Jumwa mashtaka dhidi yake.
Jaji Onginjo amesema Jumwa atahitaji kufika Mahakama kama shahidi wa kesi ya mauaji inayomkabilia Geoffrey Otieno Okuto ambaye awali alikuwa mlinzi wake wa kibinafsi alipokuwa mbunge wa Malindi wakati wa tukio hilo la mauaji lililotokea.
Itakumbukwa kwamba Jumwa na Okuto walishtakiwa baada ya kushuhudiwa kuusika na mauaji ya mfuasi wa chama cha ODM mwendazake Jola Ngumbao baada ya rabsha za kisiasa kuzuka wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi.