Picha kwa hisani –
Spika wa bunge la kaunti ya Tana River Michael Justin Nkaduda amepata afueni ya muda baada ya mahakama inayoshughulikia mizozo ya wafanyakazi kaunti ya Mombasa kusitisha mchakato wa kumtimua mamlakani.
Akitoa uamuzi huo Jaji wa mahakama hiyo Byram Ongaya amewaagiza mawakili wa Nkaduda kuwasilisha nakala maalum kutoka kwa mahakama hiyo katika bunge kaunti ya Tana River kabla ya tarehe 14 ya mwezi Mei.
Jaji Ongaya amewaagiza pia mawakili wa bunge la kaunti hiyo kuwasilisha majibu yao kwa mahakama hiyo kufikia tarehe 25 ya mwezi Mei mwaka huu kabla ya kesi hiyo kuanza kusikizwa mnamo Juni tarehe mbili mwaka huu.
Bunge la kaunti Tana River siku ya Jumanne lilimtimua mamlakani Spika Nkaduda kutokana na utepetevu, matumizi mabaya ya mamlaka na ukosefu wa nidhamu.
Jumla ya wajumbe 18 walipitishwa hoja ya kumtimua Nkaduda wakisema hafai kuendelea kushikilia wadhfa wa Spika katika kaunti ya Tana River.