Story by Deric Otieno-
Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa tuhuma za uharibifu wa mali.
Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka wa 2021 katika kijiji cha Chifusini eneo la Kinango kaunti ya Kwale Haranga Chiguzo Saidi alisababisha uharibifu wa mali ya kibinafsi ya Ruwa Chiguzo Fulusi yenye thamani ya shilingi 91,200 kwa kulisha mifugo kwenye shamba la Chiguzo.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Christine Auka mshtakiwa amekana shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 au shilingi elfu 20 pesa taslimu.
Kesi yake itatajwa tarehe 26 mwezi Juni mwaka wa 2022.