Story by Deric Otieno –
Mwanaume wa umri wa makamu amefikishwa katika mahakama ya Kwale kwa tuhuma za wizi.
Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 20 mwezi Machi mwaka wa 2022 katika kijiji cha Mwamambi eneo la Diani kaunti ya Kwale, mshukiwa kwa jina Sebastian Ibelia anadaiwa kumuibia Frankline Luvavali Mudogo, nguzo za nyaya za umme zenye thamani ya shilingi 26,400 na mlango wa mbao wenye thamani ya shilingi 15,000.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido, mshukiwa huyo amekana shtaka hilo na akaachiliwa kwa shilingi 30 pesa taslimu.
Kesi yake itatajwa tarehe 19 mwezi wa Aprili mwaka huu.
Watu wa aina ya tabia izo wanapaswa kufungwa ili wawe funzo kwa wengine wa tabia kama izo