Story by Fatuma Chai –
Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa tuhma za kunajisi mtoto wa umri wa miaka 15.
Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 17 mwezi Januari mwaka huu Mwanamume huyo kwa jina Bakari Rumba alitekeleza uovu huo akiwa katika kijiji cha Wamasa eneo la Kinango kaunti ya Kwale.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Lilian Lewa mshukiwa amekana shtaka hilo na akaachiliwa kwa dhamana na shilingi laki nne na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itatajwa mnamo tarehe 31 mwezi Januari mwaka huu katika Mahakama hiyo.