Story by Rasi & Fatuma –
Mwanamume wa umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa tuhuma za kumyanyasa kingono msichana wa miaka 16.
Katika shtaka la kwanza, Mahakama imeelezwa kwamba mnamo tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu mwanamume huyo kwa jina Hamisi Juma Garash alipenyeza vidole vyake kwenye sehemu za siri za msichana huyo akiwa katika mtaa wa Blue Jay eneo la Diani kaunti ya Kwale.
Katika shtaka la pili, mshtakiwa ametuhumiwa kwa kutekeleza kitendo kisichokua na heshima kwa kushika matiti ya msichana huyo aliye na umri mdogo.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido mshukiwa amekanusha mashtaka yote mawili na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi itatajwa tarehe 16 mwezi huu katika mahakama hiyo ya Kwale.