Story by Lauren Mbodze-
Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa tuhuma za kupiga na kujeruhi.
Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 10 mwezi Aprili mwaka huu katika kijiji cha Mwambugu eneo la Diani kaunti ya Kwale mshukiwa kwa jina Hamisi Bakari alimpiga na kumsababishia majeraha Aisha Suleiman Mwachuuza.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Zacharia Kiongo mshukiwa amekana shtaka hilo na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 au pesa taslimu shilingi elfu 20.
Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 5 mwezi Mei mwaka huu.