Story by Taalia & Chiro-
Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mwanamke mmoja katika eneo la Kona ya Musa kaunti ya Kwale.
Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 1 mwezi Januari mwaka huu mwanamume huyo kwa jina George Omondi alimpiga na kumsababishia majeraha Tabitha Mwangeka.
Akiwa mbele ya Hakimu Lilian Lewa, mshtakiwa amekubali shtaka dhidi yake huku Mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi wake tarehe 24 mwezi Januari mwaka huu.