Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa kosa la kupatikana akiwa amejihami kwa kisu tayari kutekeleza wizi.
Mahakama imeafiriwa kuwa mnamo tarehe 11 mwezi Aprili mwaka huu katika eneo la Manyatta kule Diani kaunti ya Kwale, mwanaume huyo kwa jina Martin Nguvu Kavaya alionekana na Everlyne Wesonga akiwa katika boma la jirani akivuruta chuma.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Patrick Wambugu, mshukiwa amekubali shtaka la kupatikana na kisu hicho na kujitetea mbele ya mahakama hiyo, akisema kazi yake ni kuokota mikebe na hutumia kisu hicho kukatia minyaa ya kufungia kuni za biashara.
Hata hivyo Mahakama imeagiza maafisa wa kurekebisha tabia kutaarisha ripoti na kuiwasilisha Mahakamani kabla ya Mahakama kutoa uamzi wake.
Kesi hiyo itataijwa tarehe 29 mwezi huu wa Aprili.