Story by Rasi/Mwinyi –
Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakama ya Kwale kwa kosa la kuendesha gari barabarani bila vibali.
Mahakama imeafiriwa kwamba mnamo tarehe 7 mwezi huu katika barabara ya Ukunda -Msambweni Paul Thiong’o ambaye alikuwa derava aliendesha gari bila vibali hitajika vya kuwa barabarani.
Akiwa mbele ya Hakimu mkaazi wa Mahakama ya Kwale Christian Auka mshtakiwa amekubali kosa hilo na kutozwa faini ya Shilingi elfu 10 au kifungo cha mwezi mmoja gerezani.
Hata hivyo jamaa huyo ana siku 14 za kukata rufaa kama hajaridhishwa na umauzi huo.