Story by Rasi Mangale
Mahakama ya Kwale imemhukumu kifungo cha mwezi mmoja gerezani raia wa Ethiopia baada ya kupatikana humu nchini kinyume cha sheria.
Mahakama imearifiwa kwamba Abraham Bedore alipatakana humu nchini mnamo tarehe 14 mwezi huu katika eneo la Vigurungani kwenye barabara ya Kinango-Samburu bila ya hati ya usafiri.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kwale Lilian Lewa, mshtakiwa amekiri kosa hilo na Mahakama ikaagiza raia huyo wa Ethiopia kutumikia kifungo hicho cha mwezi mmoja gerezani na kisha kurudishwa kwao baada ya mshtakiwa huyo kulalamikia hali yake ya kiafya.
Hata hivyo mshtakiwa ana siku 14 za kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama.