Mahakama ya mjini Kwale imempa kifungo cha mwaka mmoja gerezani mwanamume mmoja baada ya kukabili kutekeleza shtaka la wizi.
Mahakama imerifiwa kuwa mnamo tarehe 9 mwezi Aprili mwaka huu katika kijiji cha Ng’ombeni eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale, Mshukiwa kwa jina Baraka Abdallah Ramoyoni alitekeleza kitendo hicho.
Katika shtaka la kwanza, mshukiwa anadaiwa kuiba redio yenye thamani ya shilingi 8,000 na pesa taslimu shilingi 6,800 ikiwa ni mali ya Mwendee Mbithi.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Patrick Wambugu, mshukiwa amekubali shtaka hilo la kwanza na Mahakama ikimpa kifungo cha mwaka mmoja gerezani.
Katika shtaka la pili la kutishia kumuua mlalamishi wa kesi hiyo, mshukiwa amekana shtaka hilo huku kesi hiyo ikipangwa kutajwa tarehe 27 mwezi huu na kusikiliza tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu.