Story by Mwanaisha Soza-
Mshukiwa wa kesi ya unajisi Suleiman Musa Kambirwa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani baada ya uchunguzi wa kesi hiyo kubainika wazi kwamba alitekeleza kitendo hicho.
Hakimu mkuu wa Mahakama ya Kwale Joe Omido ameagiza mshukiwa huyo kutumikia kifungo chake katika gereza la Shimo la Tewa katika kaunti ya Mombasa.
Awali kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mshukiwa alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Christine Auka kabla ya kesi hiyo kuhamishiwa Hakimu mkuu wa Mahakama hiyo Joe Omido.
Mahakama iliarifiwa kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 12 mwezi Mei mwaka wa 2019 katika kijiji cha Malalani eneo la Diani kaunti ya Kwale kwa mtoto wa miaka 3 baada ya kumshurutisha amnyonye sehemu nyeti.
Hata hivyo mshukiwa na hadi siku 14 za kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama.