Story by Rasi Mangale –
Mahakama ya Kwale imetatoa hukumu dhidi ya mshukiwa wa ulaghai kwa jina Patel Minaj Kumar siku ya Alhamis tarehe 9 mwezi huu.
Patel amepatikana na hatia ya kuilaghai shule ya msingi ya wanafunzi wanaoishi na changamoto za ulemavu wa akili ya Kwale takriban shilingi 10,425 mnamo tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2021.
Mahakama imearifiwa kwamba mshukiwa huyo aliahidi kwamba angeisambazia shule hiyo bidhaa kutoka kampuni ya Mombasa Cement ikiwemo chakula, kuwajengea ua na kuwasadia watoto wasiojiweza, akijuwa wazi kwamba alikuwa anailaghai shule hiyo.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido, mshukiwa amekubali makosa yake na Mahakama ikaagiza azuiliwe hadi siku ya Alhamsi tarehe 9 mwezi huu wakati atakaposomewa hukumu yake.