Story by Deric/Rachel –
Mwanaume wa umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama ya Kwale akikabiliwa na shtaka la kuvunja na kuharibu mali.
Mahakama imearifiwa kwamba kati ya tarehe 17 na 28 mwezi wa Februari mwaka huu katika eneo la Kigato gatuzi ndogo la Matuga kaunti ya Kwale mshukiwa kwa jina Rashid Mwinyi Simba anadai kutekeleza kitengo hicho.
Katika ushahidi uliowasilishwa Mahakamani mshukiwa anadaiwa kuvunja na kuharibu madirisha matatu yenye thamani ya shilingi elfu 20 ambayo ni mali ya Hemed Ramadhan Mwaguzo.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Lilian Lewa mshukiwa amekana shtaka hilo na akaachiliwa kwa dhamana ya elfu 50 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho ama pesa taslimu shilingi elfu 10.
Kesi yake itasikizwa tarehe 21 mwezi Mechi mwaka huu