Story by Rasi & Mwanaisha-
Mahakama ya Kwale imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tano au pesa taslimu shilingi laki mbili mshukiwa mmoja wa kughushi stakabadhi binafsi.
Mshukiwa huo kwa jina George Odhiambo Otieno ambaye amefikishwa katika Mahakama hiyo akidaiwa kwamba mnamo tarehe 21 mwezi Septemba mwaka 2019 akiwa na wenzake ambao hawakufika Mahakamani walighushi stakabidhi binafsi.
Otieno na wenzake wanadaiwa kwamba walighushi barua ya marekebisho ya Katiba ya Serve Kenya Ministries ili isomeke kama Restoration Ministries huku wakidai kwamba ilikuwa imetiwa sahihi na Katibu wa Serve Kenya Ministries James Muthee Njau.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido, mshukiwa amekana shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana hiyo huku kesi hiyo ikipangwa kutajwa tena tarehe 13 mwezi huu wa Septemba.