Mahakama ya Kwale imemhukumu mzee wa miaka 74 kifungo cha miaka 5 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kosa la Unajisi.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Kwale hiyo Joe Omido amesema katika ushahidi uliowasilishwa Mahakamani umeonyesha wazi kwamba mshukiwa Hamisi Juma Mahendo Zani alitekeleza kitendo hicho.
Hakimu Omido amesema ni makosa mkubwa kwa mtu yeyote kumnajisi mtoto badala yake kila mmoja anafaa kumthamini mtoto na kumpa haki zake za kimsingi na wala sio kumtendea unyama.
Awali Mahakama iliarifikiwa kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto wa kike wa miaka 10 mnamo tarehe 6 mwezi Disemba mwaka 2015 katika kijiji cha Tsimba eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale.
Mshtakiwa alikuwa tayari anatumikia kifungo cha maisha gerezani na akakata rufaa mbele ya mahakama kuu ambapo ilimrudisha rumande kwa miaka 6 kabla ya hukumu yake kupunguzwa baada ya kuiomba Mahakama kumpunguzia adhabu hiyo.
Hata hivyo mshtakiwa na mda wa siku 14 za kutaka rufaa iwapo hajaridhika na uamuzi huo wa Mahakama wa kifungo cha miaka 5 gerezani.