Story by Derick & Lauren –
Mahakama ya Kwale imemhukumu kifungo cha miezi 18 gerezani mwanaume wa umri wa makamu baada ya kupatikana na hatia ya kuuza Mihadarati aina ya bangi.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Kwale Lilian Lewa, amesema ni makosa kwa mtu yeyote yule kuendeleza biahsara haramu ya Mihadarati, akidai kwamba kifungo hicho kitakuwa funzo kwa watu wengine.
Kabla ya hukumu hiyo, Mahakama iliarifiwa kwamba jamaa huyo kwa Ramadhan Malumwe Salim alipatika na misokoto minne ya bangi pamoja na jiwe moja la kutengeneza bangi hiyo zote zikiwa za thamani ya shilingi elfu 7 katika kijiji cha Mabriver eneo la Tiwi kaunti ya Kwale mnamo tarehe 9 mwezi Februari mwaka huu.
Hata hivyo mshukiwa ana siku 14 za kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama ama atumikie kifungo chake katika gereza la shimo la Tewa kaunti ya Mombasa.