Story by Derrick/Rachel –
Mahakama ya Kwale imemhukumu kifungo cha nje cha miaka mitatu mtoto wa kike wa umri wa miaka 14 baada ya kupatika na biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Hakimu wa Mahakama hiyo Lilian Lewa amesema mtoto huyo atatumikia kifungo chake katika kituo cha watoto cha kurekebisha tabia cha Nakuru Probation Hostel ili kumtenganisha mtoto huyo na walanguzi wakuu wa biashara hiyo haramu.
Mahakama imeeleza kwamba uamuzi huo umefanywa ili kumpa fursa mtoto huyo kuendelea na masomo sawa na kumrekebisha tabia huku akiwa chini ya ulinzi wa maafisa wa kurekebisha tabia katika kituo hicho huku Nakuru.
Hata hivyo Mahakama iliarifiwa kwamba mtoto huyo wa kike wa umri wa miaka 14 alikuwa akiendeleza ngono biashara huku akiendeleza ulanguzi wa dawa za kulevya licha ya kuwa na umri mdogo.