Story by Rachel Weru –
Mahakama ya Kwale imemhukumu kifungo cha miaka 7 gerezani mwanamume wa umri wa makamu baada ya kupatikana na hatia ya uwizi wa mabavu pamoja na kosa la kujaribu kutekeleza ubakaji.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa Makakama ya Kwale Joe Omido amesema ni makosa makubwa kwa mtu yeyote kutekeleza wizi wa mabavu pamoja na kujaribu kutekeleza ubakaji na adhabu hiyo itakuwa funzo kwa wengine.
Awali kabla ya hukumu hiyo, mshukiwa alidaiwa kutekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 6 mwezi Disemba mwaka wa 2018 kwa kuvunja na kuingia kwa nguvu katika nyumba ya Rukia Zaitun pamoja na kutekeleza jaribio la ubakaji.
Hata hivyo mshukiwa ana mda wa siku 14 za kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama ama atumikie kifungo chake katika gereza la Shimo la Tewa kaunti ya Mombasa.