Story by Fatuma Chai –
Mahakama ya Kwale imemhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani mwanamume umri wa miaka 20 baada ya kupatikana na kosa la unajisi.
Mahakama imearifiwa kwamba mshukiwa kwa jina Shaban Mwachome Suleiman, alitekeleza kitendo hicho kwa mtoto wa umri wa miaka 17 katika eneo la Mwamanga kule Diani kaunti ya Kwale kati ya tarehe tofauti mwezi Septemba mwaka 2017 na mwezi Septemba mwaka 2018.
Katika uamuzi wake Hakimu mkaazi Christine Auka amesema mshukiwa huyo atatumikia kifungo chake katika gereza la Shimo la Tewa katika kaunti hiyo Mombasa ili iwe funzo kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Hata hivyo mshukiwa amepewa mda wa siku 14 kukata rufaa iwapo hajaridhika na uamuzi wa Mahakama.