Story by Mwanaisha/Fatuma-
Mahakama ya Kwale imeagiza kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kinango mshukiwa wa biashara haramu ya pembe za ndovu baada ya kukana shtaka dhidi yake.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido mshukiwa kwa jina Nyae Mrisa Kengo anadaiwa kwamba mnamo tarehe 11 mwezi huu katika kijiji cha Vyogato kaunti ya Kwale alipatikana na pembe tano za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni 1.7.
Hata hivyo mshukiwa wa pili katika kesi hiyo Mwanaisha Mchedzua Chiliku alikubali kosa lake na Mahakama akimuagiza kufikiria kwa kina kwani adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha miaka 7 au faini ya shilingi milioni 3.
Kesi hiyo itatajwa na kusikizwa tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.