Story by Our Correspondents-
Mahakama kuu jijini Nairobi imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na mbunge wa Sirisia John Waluke dhidi ya kesi inayomkabili ya sakata ya ufisadi ya shilingi milioni 297 za bodi ya mazao na nafaka nchini NCPB inayomkabili.
Jaji wa Mahakama hiyo Esther Maina amesema rufaa hiyo haina uzito wa kubatilisha uamuzi uliyotolewa na Mahakama ya inayoangazia maswala ya ufisadi chini ya Hakimu wa Mahakama hiyo Elizabeth Juma kwamba anafaa kulipa faini ya shilingi 727,725,562 ama atumikie kifungo cha miaka 67 gerezani.
Waluke pamoja na Judy Wakhungu walikuwa wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 na shilingi milioni 20 mtawalia mwaka wa 2020 wakati kesi hiyo ilipowasilishwa Mahakakani na tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC.
Mbunge huyo ambaye alichaguliwa kwa muhula watatu italazimika kutumikia kifungo hicho cha miaka 67 gerezani iwapo atashindwa kulipa faini ya shilingi 727,725,562 huku Judy Wakhungu akipewa kifungo cha miaka 69 ama faini ya shilingi 707,725,562.
Wawili hao wanadaiwa kufuja fedha za umma kwa kujipatia zabuni ya shilingi milioni 297 kinyume cha wakati wakifanyakazi katika bodi ya mazao na nafaka nchini NCPB.
Hata hivyo wana mda wa siku 14 za kukata rufaa iwapo hawajaridhika na uamuzi huo ama watumikia kifungo hicho gerezani.