Story by Our Correspondents –
Mahakama kuu imedinda kusitisha hukumu ya miezi minne aliyopewa mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI, George Kinoti.
Mahakama hiyo imeagiza swala hilo kusikizwa siku ya Alhamis kwani kesi hiyo ina uzito na inahitaji uamuzi wa dhararu.
Uamuzi huo wa Mahakama kuu umetokana na ombi lililowasilishwa na Mwanasheria mkuu nchini Paul Kihara aliyefika Mahakama na kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu hukumu hiyo sawa na kutaka hukumu hiyo kusitishwa kwa mda.
Hata hivyo juma lililopita Jaji wa Mahakama kuu Antony Murima alitoa uamuzi wa kutiwa nguvuni na kutupwa gerezeni kwa miezi minne Kinoti baada ya kukaidi agizo la Mahakama la kurejesha bunduki za mfanyibiashara maarufu nchini Jimmy Wangiji.
Hata hivyo baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa ushirikiano na baadhi ya vijana jijini Nairobi wamejitokeza na kumpa makataa ya saa 48 Jaji mkuu nchini Martha Koome kuingilia kati swala hilo na kusitisha agizo la kutupwa gerezani Kinoti.