Story by Charo Banda –
Mahakama kuu ya Malindi ameagiza kuzuiliwa rumande kwa washukiwa watatu wa mauaji ya mfanyibiashara maarufu mjini Malindi Mohammed Nassir Juma hadi Oktoba 28 mwaka huu ambapo watatu hao watafikishwa tena Mahakamani.
Jaji wa Mahakama hiyo Stephen Githinji ametoa agizo hilo na kusisitiza watatu hao kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi baada ya upande wa mashtaka kuiomba Mahakama hiyo kuipa mda wa juma moja kukamilisha uchunguzi wao.
Jaji Githinji amewaagiza pia maafisa wa usalama kuwapa ulinzi wa kutosha mashahidi kwenye kesi hiyo ili kuzuia washukiwa kuhitilafiana na kesi hiyo.
Awali kabla ya agizo hilo, Mahakama iliarifiwa kwamba watatu hao akiwemo Nelson Wanje Mugaya, Henry Wanje Karani, na Amos Kiponda Charo walitekeleza kitendo hicho cha kinyama mnamo tarehe 12 mwezi Agosti mwaka huu katika kijiji cha Kolonje eneo la Jilore katika kaunti ndogo ya Malindi.