Picha kwa hisani –
Mahakama kuu ya Garsen imemuachilia kwa dhamana ya shilingi nusu milioni ama pesa taslimu shilingi laki tatu, Mwakilishi wa Wadi ya Mkomani kaunti ya Lamu Yahya Ahmed Shee baada ya kukata rufaa dhidi ya kesi iliokuwa ikimkabili.
Jaji wa Mahakama ya Garsen Reuben Nyakundi ametoa uamuzi huo baada ya Shee anayefahamika kwa jina maarufu Basode akiwa tayari amehudumu gerezani kwa majuma matatu baada ya kupewa kifungo cha miaka 5 na Mahakama ya Lamu
Hii ni baada ya Mahakama ya Lamu kumpata na hatia Basode ya kujaribu kumtorosha mlanguzi wa dawa za kulevya aliyekuwa amehukumiwa na Mahakama ya Lamu kifungo cha miaka 20 gerezani, tukio lililofanyika tarehe 2 ya mwezi Juni mwaka wa 2017.
Wafuasi wa Kiongozi huyo wameandamana wakifurahia hatua hiyo huku wakidai kuwa Basode anapigwa vita kisiasa na wapinzake wake akiwemo Gavana wa Lamu Fahim Twaha kutokana na uwajibikaji wake katika bunge la kaunti ya Lamu.