Picha kwa hisani –
Mahakama kuu imetangaza kuwa wazi kiti cha ubunge cha eneo la Gatundu Kaskazini.
Akitoa uamuzi huo jaji Weldon Korir amesema mbunge anaeshikilia kiti hicho Wanjiku Kibe alichaguliwa pasi na kujiuzulu wadhafa wa uwakilishi wadi aliyoushikilia na kwamba hatua hio ni kinyume cha sheria.
Jaji Korir ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kupanga upya uchaguzi mdogo wa kiti hicho akimtaka naibu msajili kuwasilisha uamuzi huo wa mahakama kwa spika wa bunge la kitaifa ili achukue hatua zifaazo.
Hayo yamejiri baada ya aliyekuwa mbunge wa a eneo bunge hilo Clement Kung’u Waibara kuwasilisha kesi mahakamani kupinga uchaguzi wa Wanjiku Kibe akidai kwamba ulikiuka sheria.