Picha kwa hisani –
Baada ya kuzindua ngoma yao mpya Otile brown na Ali kiba kwa jina in love, wengi sasa wanasema
hivyo vilikuwa Vita vya vocals Kati ya mkali wa RnBs nchini Kenya otile na mfalme wa bongo fleva king
kiba, huku wengi wakitoa maoni tofauti tofauti.
Kama ilivyo kawaida kwa ngoma za otile na pia ali kiba, wimbo huo umefanya poa kwa mtandao wa
YouTube huku ukitazamwa na zaidi ya watu laki nne na elfu sitini ndani ya saa 20. Huku tayari ukishikilia nambari mbili kwenye trends za YouTube nchini.
Kumbuka miaka mitatu iliyopita, wimbo wa Ali Kiba uliweka rekodi ya kuwa wimbo iliofikisha zaidi ya
views milioni moja ndani ya masaa 24.
Otile ambaye ametamba Sana na ngoma ya Dusuma aliyomshirikisha Meddy kutoka Rwanda na pia
Watoto na Pombe aliyofanya na Mejja na Magix enga, amepongezwa na mashabiki wake kwa kutengeza
collabo hizo.
Hivi, kwa maoni yako kati ya Otile Brown na Ali Kiba nani kafunika?