Jumla ya magunia 1,147 ya sukari yametekezwa baada ya sukari hiyo kubainika kuwa kamwe sio nzuri kwa matumizi ya binadamu.
Mshirikishi mkuu wa Serikali ya kitaifa Kanda ya Pwani John Elungata amesema magunia mengine laki mbili na elfu themanini ya sukari isiyofaa kwa matumizi ya binadamu na yanayohifadhiwa katika bohari moja Mjini Mombasa yatachomwa hivi karibuni.
Elungata amesema msako mkali dhidi ya bidhaa ghushi zinazoingizwa katika bandari ya Mombasa au zinazouzwa katika masoko ya Ukanda wa Pwani umeiamrishwa.
Mshikishi huyo amesema jopo hilo limekuwa likiendeleza oparesheni hiyo ya kusaka bidhaa bandia kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na sasa linawalenga wale wanaoingiza bidhaa hizo humu nchini.
Magunia hayo ya sukari ya kilo hamsini yaliingizwa humu nchini kutoka nchini Brazil na Kampuni ya Lumira General Trading.