Story by Our Correspondents–
Wizara ya Elimu nchini imefanya mabadiliko ya tarehe ya kufunguliwa kwa shule na kuchapisha rasmi katika gazeti la serikali.
Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema shule sasa zitafunguliwa rasmi tarehe 18 siku ya Alhamis baada ya kuafikiana na wadau wa sekta ya elimu nchini.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Magoha amesema hatua hiyo imejiri ili kupeana nafasi kwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukamilisha shughuli yao ya kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Hata hivyo amewataka wazazi kuwatayarisha watoto na mapema kuhusu maswala ya elimu.