Story by Our Correspondents –
Waziri wa Elimu nchini Prof. George Magoha amesema mtaala mpya wa elimu wa CBC utaendelea kutekelezwa shuleni licha ya baadhi ya wazazi na wadau wengine wa maswala ya elimu kuupinga mtaala huo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya ziara ya kielimu katika kaunti ya Kakamega, Waziri Magoha amesema japo kumeshuhudiwa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mtaala huo serikali imejipanga vyema.
Magoha hata hivyo amewapuuza wale wote wanaoutilia shaka mtaala huo, akisema ni lazima wadau wote wa sekta ya elimu na wazazi kuungana ili kuwasaidia wanafunzi shuleni.
Wakati uo huo amedokeza kwamba serikali bado inashuhulikia swala la muundo msingi katika shule mbalimbali nchini ili kukimu idadi kubwa ya wanafunzi.