Story by Our Correspondents –
Wazira wa Elimu nchini Prof George Magoha amewarai viongozi wa chama cha Walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET kufutilia mbali ilani walioitoka kwamba wataandaa mgomo wa walimu kuanzia wiki ijayo.
Waziri Magoha amesema viongozi wa walimu wanafaa kusitisha mpango huo na kuruhusu majadiliano ya kina kuhusu matakwa ya walimu ili yatatulikwe kwani mpango wa kushiriki mgomo sio suluhu la kutatua changamoto zinazowakabili walimu.
Akizungumza katika kaunti ya Kericho baada ya kufanya ziara ya kielimu katika kaunti hiyo, Magoha amesema japo walimu wana haki kikatiba ya kushiriki mgomo itakuwa sio jambo jema kwa walimu hao kushiriki mgomo wakati wa mitihani ya kitaifa.
Wakati uo huo amewahakikisha wanafunzi usalama wa kutosha wakati wa mitihani hiyo huku akisema tayari maandalizi ya mitihani inaendelea kabla ya mitihani hiyo kuanza rasmi mwezi ujao wa Machi.