Picha kwa hisani –
Baraza la magavana nchini limetoa mapendekezo wanayotaka yajumuishe kwenye ripoti ya BBI,ikiwemo kuongezwa nguvu kwa masenete ili wawe na uwezo wa kujadili na kupitisha kuunda sheria mbali mbali nchini.
Akizungumza kwenye kongamano la magavana na wawakilishi wadi la kujadili ripoti ya BBI huko Naivasha,mwenyekiti wa magavana Wycliffe Oparanya vile vile amesema kunapaswa kuidhinishwa wadhfa wa naibu waziri na watateuliwa kutoka bunge la kitaifa.
Oparanya vile vile amesema magavana wanapendekeza mfumo wa Jumuia za kaunti kujumuishwa katika ripoti hio ya BBI, na kwamba serikali za kaunti zinapaswa kupewa idhini ya kuchukua mikopo ya kuidhinishia maendeleo miongoni mwa mapendekezo mengine.
Kwa upande wao wabunge wa kike nchini wanaogemea upande wa Rais Uhuru Kenyatta wakiongozwa na mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko wamesema wanaunga mkono ripoti ya BBI kwani ni kupitia ripoti hio, jinsia zote mbili zitajumuishwa kwenye suala la uongozi.