Magavana wa kaunti za Pwani wamesisitiziwa kuhakikisha kwamba kaunti zao hazikabiliwi na migogoro.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika linalopigania maswala ya amani hapa Pwani la Kenya Community Support Centre-KECOSCE Bi Phyllis Muema amesisitiza umuhimu wa Magavana kupigania amani na uiano Katika kaunti zao ili kuizuia mizozo baina ya jamii.
Akizungumza Mjini Mombasa, Bi Muema amewahimiza Magavana kubuni Idara za amani, usalama na uiano katika Kaunti zao ili kuliangazia kwa kina swala la amani mashinani badala ya kusubiri hadi uchaguzi mkuu unapowadia.
Afisa huyo amedai kwamba magavana wamewachia jukumu hilo Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, hali inayochangia pakubwa kuzuka kwa migogoro katika maeneo mbalimbali Pwani.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.