Story by Winne Chitaka-
Vugu vugu la Fast Action Business Community kanda ya pwani linawataka magavana wote sita wa kaunti za pwani kuwekeza zaidi katika kuimarisha sekta ya afya katika ukanda huu.
Mwenyekiti wa vuguvugu hilo Salim Karama amesema wakaazi wa Pwani wanapitia changamoto nyingi wakati wanapotafuta huduma za afya hali ambayo imepelekea watu wengi kupoteza maisha yao kwa kukosa kupata huduma za afya kwa haraka.
Karama aidha anapendekeza gharama ya huduma hizo iwe ya chini ambayo kila mkaazi anaweza kugharamia huku akizitaka serikali za kaunti kuwashirikisha wakaazi wote bila ya kuwabagua kikabila, kidini, kijinsia wala rangi.