Magavana wa kaunti za Pwani wamehimizwa kuidhinisha mipangilio ya kuzifufua taasisi zote za kiufundi mashinani ili kuwawezesha Vijana kusomea taaluma mbalimbali.
Mwenyekiti wa Shirika linalohusika na Masuala ya Biashara na Viwanda Nchini Kenya National Chamber of Commerce & Industry Bi Rukia Rashid amesema kwamba japo sekta ya elimu haijagatuliwa Magavana wanapaswa kushirikiana na Maseneta pamoja na Wawakilishi wa kike katika Kaunti kuweka mikakati ya kuzifufua na kuziboresha taasisi hizo.
Akizungumza Mjini Mombasa, Bi Rukia amesema kwamba taasisi nyingi za kiufundi zilizovuma mbeleni sasa zimesalia magofu huku Vijana wasiokuwa na uwezo wa kujiunga na vyuo vikuu wakikosa namna ya kupata ujuzi ili kujibunia ajira binafsi.
Taarifa na Gabriela Mwaganjoni